• HABARI MPYA

  Friday, November 05, 2021

  AZAM, GSM NA WENGINE WAICHANGIA TAIFA STARS BILIONI 1.6


  WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanikiwa kukusanya michango kisi cha Sh. Bilioni 1.6 kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa nchini kwa ajili ya kampeni ya timu ya taifa ya Tanzania kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar.
  Miongoni mwa wadau walioshiriki hafla hiyo ni kutoka kampuni za GSM, Taifa Gas, Azam, CRDB, NBC, Lake Oil, Star Oil, K4 Security na Kambiaso.
  Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu.


  Taifa Stars inatarajiwa kumenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Novemba 11 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia kabla ya kukamilisha michezo ya kundi hilo kwa kumenyana na Madagascar Novemba 14 Jijini Antananarivo.
  Kwa sasa Taifa Stars inaongoza Kundi J kwa pointi zake saba ikiizidi wastani wa mabao Benin, wakifuatiwa na DRC pointi tano na Madagascar pointi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM, GSM NA WENGINE WAICHANGIA TAIFA STARS BILIONI 1.6 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top