• HABARI MPYA

  Friday, November 05, 2021

  WAZIRI MKUU AKUTANA NA WACHEZAJI TAIFA STARS


  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars kuelekea mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Novemba 11 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu amewahamasisha wachezaji hao kujituma kuhakikisha wanashinda michezo yao miwili ya mwisho ili waende hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya Qatar mwakani.
  Baada ya mechi dhidi ya DRC Dar es Salaam, Taifa Stars itasafiri kuifuata Madagascar kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Kundi J Novemba 14 Jijini Antananarivo.


  Kwa sasa Taifa Stars inaongoza Kundi J kwa pointi zake saba ikiizidi wastani wa mabao Benin, wakifuatiwa na DRC pointi tano na Madagascar pointi tatu.
  Ikumbukwe washindi wa makundi 10 watamenyana baina yao kupata wawakilishi watano wa Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU AKUTANA NA WACHEZAJI TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top