• HABARI MPYA

  Friday, November 12, 2021

  WAKONGO WAENDELEA KUING’ARISHA YANGA SC


  YANGA SC imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya KMKM katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  KMKM walitangulia kwa bao la Optatus Lupekenya dakika ya 20, kabla ya Yanga kuzinduka kwa mabao ya Wakongo, winga Jesus Moloko 27 na Fiston Mayele dakika ya 85.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kirafiki kwa Yanga baada ya Jumanne kushinda 1-0 hapo hapo Amaan, bao la Mkongo mwingine, Heritier Makambo.
  Yanga iliwasili Jumanne Zanzibar kuweka kambi ya wiki moja kipindi hiki cha mapumziko mafupi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAKONGO WAENDELEA KUING’ARISHA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top