• HABARI MPYA

  Saturday, November 27, 2021

  PRISONS YAIPIGA NAMUNGO 3-1, MCC NA KMC 2-2

  WENYEJI, Tanzania Prisons wamepata ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Namungo FC mabao 3-1 jioni ya leo Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Mabao yote ya Tanzania Prisons leo yamefungwa na mshambuliaji Jeremiah Juma dakika ya nne, 11 na 26, wakati bao pekee la Namungo FC limefungwa na mshambuliaji Mrundi, Bigirimana Blaise dakika ya 68.
  Kwa ushindi huo, Prisons inafikisha pointi nane na kujiinua hadi nafasi ya nane, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake sita katika nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 13.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji Mbeya City wamelazimishwa sare ya 2-2 na KMC Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Paul Nonga dakika ya nane na Richardson Ng'ondya dakika ya 67 na ya KMC yamefungwa na Matheo Anthonyu dakika ya 13 na Mohamed Samatta dakika ya 86.  
  Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tatu, wakati KMC inafikisha pointi sita na inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya 16 baada ya timu zote kucheza mechi saba.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAIPIGA NAMUNGO 3-1, MCC NA KMC 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top