• HABARI MPYA

  Sunday, November 28, 2021

  SIMBA YAITANDIKA RED ARROWS 3-0


  SIMBA SC imejiweka katika nafasi nzuri ya kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, nyota wa mchezo alikuwa ni kiungo Mghana, Bernard Morrison aliyefunga mabao mawili na kuseti moja.
  Mchezaji huyo wa zamani wa wapinzani wa jadi, Yanga alifunga bao la kwanza dakika ya 17 na la tatu dakika ya 78, wakati la pili 'alimtafunia' mshambuliaji Mnyarwanda mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere aliyefunga dakika ya 20.
  Timu hizo zitarudiana Desemba 5 Jijini Lusaka na mshindi wa jumla atakwenda hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAITANDIKA RED ARROWS 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top