• HABARI MPYA

  Friday, November 19, 2021

  PRISONS YAPATA USHINDI WA KWANZA WA MSIMU

  TIMU ya Tanzania Prisons imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya kuichapa Mbeya Kwanza 2-1 jioni ya leo Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Dotto Shaaban dakika ya 29 na Jeremiah Juma dakika ya 90, wakati Vedastus Mwihambi alijifunga dakika ya  26 kuipatia bao pekee Mbeya Kwanza kwenye mchezo huo.
  Prisons inafikisha pointi tano katika mchezo wa sita na kujiinua kutoka mkiani hadi nafasi ya 12, wakati Mbeya Kwanza inayopoteza mechi ya kwanza tangu ipande Ligi Kuu msimu huu inabaki na pointi zake saba za mechi sita sasa katika nafasi ya nane sasa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAPATA USHINDI WA KWANZA WA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top