• HABARI MPYA

  Wednesday, November 03, 2021

  AZAM FC YAICHAPA GEITA GOLD 1-0


  BAO pekee la mshambuliaji Mzambia. Rodgers Kola dakika ya 83 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Jumanne Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Azam FC ingeweza kuondoka na ushindi mpana kama Lusajo Mwaikenda angefunga mkwaju wa penalti dakika ya 48 ambao ulipanguliwa na kipa Khomein Abubakar kufuatia Iddi Nado kusukumwa kwenye boksi.
  Azam FC inafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya saba, wakati Geita Gold inabaki na pointi mbili katika nafasi ya 14 baada ya timu zote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA GEITA GOLD 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top