• HABARI MPYA

  Tuesday, November 30, 2021

  YANGA SC YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0


  VINARA Yanga SC wametanua uongozi wao hadi pointi tano dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 18 na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 26 akimalizia pasi ya kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto'.
  Yanga SC inafikisha pointi 19 baada ya mechi saba na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya watani wao wa jadi, Simba SC ambao wana mechi moja mkononi na kesho watawakaribisha Geita Gold Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
  Mbeya Kwanza wanabaki na pointi zao saba za mechi saba katika nafasi ya 11.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Biashara United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Mshambuliaji Adam Adam aliwatanguliza wageni, Polisi dakika ya 46, kabla ya Nassib Mpapi dakika ya 61.
  Biashara United inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya saba, wakati Polisi Tanzania inafikisha pointi 11, ingawa inabaki nafasi ya tano baada ya timu zote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top