• HABARI MPYA

  Monday, November 01, 2021

  CHOMBO REDONDO AREJESHWA TAIFA STARS

  KIUNGO mkongwe, Ramadhani Suleiman Chombo ‘Redondo’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Novemba 11, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kikos hicho kimetajwa na kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen alipozungumza na Waandishi wa Habari leo.


  Kikosi hicho kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Polisi Tz), Ramadhani Kabwili (Yanga).
  Mabeki;Shomari Kapombe (Simba), Kibwana Shomari (Yanga), Israel Mwenda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Erasto Nyoni (Simba), Dickson Job (Yanga), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Kennedy Juma (Simba), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Edward Manyama (Azam FC), Nickson Kibabage (KMC)
  Viungo; Meshack Mwamita (Kagera Sugar), Novatus Dismass (Maccabi Tel Aviv), Muzamil Yassin (Simba SC), Ramadhani Chombo (Biashara United), Zawadi Mauya (Yanga), Feisal Salum (Yanga).  
  Washambuliaji; John Bocco (Simba), Iddi Suleman (Azam FC), Abdul Suleiman (Coastal Union), Kibu Dennis (Simba), Reliant Lusajo (Namungo FC), Simon Msuva (Wydad AC) na Mbwana samatta (Royal Antwerp).

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHOMBO REDONDO AREJESHWA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top