• HABARI MPYA

  Monday, November 08, 2021

  FEISAL MCHEZAJI BORA, NABI KOCHA BORA


  KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ameteuliwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku kocha wake, Mtunisia, Nasreddine Nabi akiteuliwa Kocha Bora wa mwezi huo.
  Taarifa ya Bodi ya Ligi jioni leo imesema kwamba mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Vitalis Mayanga ameteuliwa Mchezaji Bora wa mwezi wa kwanza wa msimu, Septemba huku kocha wake, Malale Hamsini akiteuliwa Kocha Bora mwezi huo wa tisa.
  Tumaini Ikomba ameteuliwa Meneja Bora wa Uwanja mwezi Septemba kwa nzuri Uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu na Modestus Mwaluka amekuwa Meneja Bora wa Oktoba kwa kazi yake nzuri Uwanja wa Sokoine uliopo Mbeya.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEISAL MCHEZAJI BORA, NABI KOCHA BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top