• HABARI MPYA

  Tuesday, November 16, 2021

  SIMBA SC YAONGEZA KOCHA KUTOKA HISPANIA


  KLABU ya Simba imemtambulisha Mspaniola, Don Daniel De Castro Rayes kuwa kocha wake mpya wa mazoezi ya utimamu wa mwili, akichukua nafasi ya Mtunisia, Adel Zrane aliyeondolewa mwezi uliopita.
  Rayes aliyewahi kufanya kazi Politehnica Las, Rapid Bucharest za Romania na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ys Real Madrid ya kwao, Hispania atakuwa chini ya Kocha Mkuu, Mspaniola mwenzake, Pablo Franco Martin aliyewasili Jumanne iliyopita kuchukua nafasi ya Mfaransa,  Didier Gomes Da Rosa aliyeondolewa pia mwezi uliopita.
  Rayes ana Bachelor ya Physical ya Fitness Training aliyosomea katikka Chuo cha  Real Madrid.
  Makocha wengine Simba ni Mnyarwanda, Thierry Hitimana na mzawa, Suleiman Matola - maana yake timu inahitaji kocha wa makipa wa kuchukua nafasi ya Mbrazili, Milton Nienov aliyeondolewa sambamba na Gomes na Zrane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAONGEZA KOCHA KUTOKA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top