• HABARI MPYA

  Wednesday, November 10, 2021

  AZAM FC YAWAPA KOZI STEWARDS WAKE


  KLABU ya Azam FC imeendesha kozi maalumu ya askari wasimamizi wa uwanja kwenye mechi (stewards), ambayo imefungwa rasmi jana makao makuu ya timu hiyo, Uwamja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kozi hiyo imeendeshwa na Afisa Ulinzi na Usalama Viwanjani anayetambuliwa na mamlaka za soka na Serikali, ASP Mohamed Manyahe.
  Kozi hiyo ilihusisha Maafisa pekee wa ulinzi wa Azam FC, pamoja na wafanyakazi wengine ambao kwa ujumla wanapewa ujuzi huo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo kwa uweledi mkubwa.
  Katika ufungaji wa kozi hiyo, uongozi wa Azam FC uliwakilishwa na Mkurugenzi wake wa Soka, Dk. Jonas Tiboroha, aliyeambatana na nyota na Meneja wa zamani, Phillip Alando, aliyefunga kozi akimwakilisha Mwenyekiti, Nassor Idrissa 'Father'.
  Kozi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kwa hatua ya pili katika siku za usoni, lengo likiwa ni kuwanoa vilivyo askari hao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWAPA KOZI STEWARDS WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top