• HABARI MPYA

  Friday, November 19, 2021

  UCHAGUZI WA BODI DESEMBA 4 BAGAMOYO


  UCHAGUZI wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) sasa utafanyika Desemba 4, mwaka huu mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
  Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Novemba 27 mjini Kigoma, lakini taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF Alhamisi imesema kwa kutumia kanuni ya 10 (8) wameusogeza mbele uchaguzi huo na kubadili mkoa ambao utafanyika.
  Mwenyekiti wa sasa Bodi, Steven Jarvis Mnguto wa Coastal Union ndiye mgombea pekee aliyepitishwa kuwania tena nafasi hiyo baada ya kuenguliwa Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk Mshindo Mbette Msolla na wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu, huku Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ pekee akipitishwa kugombea nafasi ya Makamu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UCHAGUZI WA BODI DESEMBA 4 BAGAMOYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top