• HABARI MPYA

  Saturday, November 20, 2021

  JAMAA WA BUKOBA ASHINDA MILIONI 11 SPORTPESA  MKAZI wa Bukoba wilaya ya Muleba Juhudy Stewaty (21) ameibuka mshindi wa Jackpot Bonus baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 na kujishindia kiasi cha shilingi 11,049,185.
  Akizungumzia usindi wake Juhudy alisema “Ninafuraha kubwa sana kuibuka mshindi kwani kupitia pesa hii itanisaidia kwenye mambo mbalimbali.
  “Nilianza kucheza na SportPesa tangu mwaka 2018 hivyo ni miaka mitatu sasa na niliifahamu hii kampuni kupitia rafiki yangu wa karibu. Nilikuwa nikiona akiweka 500/- na kushinda hadi elfu 40 nikashawishika sana na kuamua kuanza kucheza.”
  “Ukiachilia ushindi huu mkubwa tangu nianze kucheza nimewahi kushinda pesa kupitia ubashiri wa mechi moja moja lakini pesa kubwa niliyowahi kushinda ni shilingi 7700 tu.”
  “Sikuwahi kukata tamaa hata siku moja kwenye kubashiri nikiamini ipo siku nitashinda Jackpot ndipo nilipoanza kuweka mikeka miwili au mitatu kwa Jackpot moja na kushinda hii bonus hatimae imekuwa hivi”
  “Mipango niliyonayo na pesa hizi ni mikubwa ikiwemo kununua viwanja nyumbani ili niweze kuwekeza, kufungua biashara ya nguo ambayo itaniendeshea maisha yangu ya kila siku na kuniingizia kipato na la mwisho kabisa ni kufunga ndoa.”
  Akizungumza upande wa SportPesa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Tarimba Abbas alisema hii ni vizuri sana kuona tunaweza kubadili maisha ya vijana wadogo na kuinua kipato chao.
  Kupitia Sportpesa tumeendelea kuwazawadia wateja wetu zawadi mbalimbali na ndio maana hata kwa wanaobashiri jackpot na wakapatia kwa usahihi kuanzia mechi 10 basi watabata bonus za viwango mbalimbali kulingana na ubashiri wao”
  “Napenda kutoa rai kwa vijana kushiriki katika michezo mbalimbali maana kubet sio uhuni bali inahitaji uelewa wa michezo na ufatiliaji pia ili uweze kupatia ubashiri wako”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JAMAA WA BUKOBA ASHINDA MILIONI 11 SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top