// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI NIYONZIMA, KUMFICHUA KWENYE SIMBA DAY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI NIYONZIMA, KUMFICHUA KWENYE SIMBA DAY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, August 01, 2017

  SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI NIYONZIMA, KUMFICHUA KWENYE SIMBA DAY

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  lSIMBA SC imemtambulisha rasmi Nahodh wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima kuwa mchezaji wake mpya akitokwa kwa mahasimu wa jadi, Yanga alipodumu kwa miaka sita.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo kwenye uzinduzi wa wiki ya Simba, Msemaji wa klabu hiyo, Haji Sunday Manara amesema kwamba Haruna tayari ni mali ya Simba na atawasili nchini kujiunga na wenzake watakaporudi kutoka Afrika Kusini walipokwenda koweka Kambi.
  “Napenda kuwaambia mashabiki na wapenzi wa klabu ya Simba kwamba, Niyonzima  tayari ni mali ya Simba na atawasili hapa nchini wikiendi hii kujiunga na wenzake pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali kwenye wiki ya Simba kabla ya Simba Day,” amesema Manara.
  Haji Manara (kushoto) akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo 
  Wakati huo huo: Klabu ya Simba imezindua rasmi wiki yake ijulikanayo Wiki ya Simba kuelekea kilele cha maazimisho ya Simba Day.
  Wiki ya Simba itakamilishwa mwa matukuo mbalimbali ikiwemo kutembelea watoto yatima, kutembelea watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo, kugawa mipira kwenye kliniki na kadhalika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI NIYONZIMA, KUMFICHUA KWENYE SIMBA DAY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top