• HABARI MPYA

  Tuesday, August 15, 2017

  SIMBA KUFANYA SEMINA YA MABADILIKO KESHO SABASABA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba kesho inatarajiwa kufanya Semina kubwa ya Wanachama wote wa klabu hiyo kuwapa elimu ya mabadiliko. 
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kwamba semina hiyo inalenga kujenga uelewa mpana zaidi juu ya muundo mpya wa uendeshwaji wa klabu hiyo.
  Manara amesema na hiyo inafuatia mabadiliko ya Katiba ya Simba yaliyofanywa na wanachama wa klabu hiyo na kusajiliwa na Msajili wa Vyama vya Michezo na Klabu nchini. 
  “Maandalizi yote ya Semina hiyo yamekamilika,na itafanyika kesho tarehe 16 mwezi wa 8 mwaka 2017, ambayo itakuwa ni Jumatano kuanzia Saa Nane na Nusu mchana (8.30)”.
  Manara amesema Semina hiyo itafanyikia kwenye ukumbi wa Mikumi uliopo kwenye eneo la maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba (PTA), Kurasini mjini Dar es Salaam. 
  “Tunawaomba wanachama wote popote walipo waje kwa wingi hapo kesho, huku klabu ikiwaomba viongozi wa Simba Wilaya ya Temeke waandae utaratibu mzuri wa kuwapokea wageni,” amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA KUFANYA SEMINA YA MABADILIKO KESHO SABASABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top