// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MZEE RUKSA’ MGENI RASMI DAR MARATHON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MZEE RUKSA’ MGENI RASMI DAR MARATHON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, August 02, 2017

  MZEE RUKSA’ MGENI RASMI DAR MARATHON

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  RAIS wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio na matembezi ya Rotary Dar Marathon yatakayo  fanyika siku ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa awamu ya kwanza, baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, mwaka huu.
  Akizungumza kweye uzinduzi wa mbio hizo leo mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa maandalizi ya Rotary kwa kushirikiana na Bank M, Catherinerose Barretto amesema kwamba lengo la mbio na matembezi hayo ni kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika hospital ya CCBRT, ambayo huhudumia matatizo mbalimbali ya ulemavu ili kuiwezesha hosptali hiyo kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.
  Rais mstaafu wa awamu ya pil, Alhaj Ally Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio na matembezi ya Rotary Dar Marathon Oktoba 14 
  Mkurugenzi wa Bank M, Jacqueline Woiso (wa pili kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Rotary Dar Marathon (kulia kwake) wakisaini mkataba wa kushirikiana katika mbio na matembezi hayo

  “Tunayo furaha kubwa kuzindua na kusaini mkataba wa kushirikiana na Bank M kama mdhamini mkuu wa matembezi ya mwaka huu na kuna mambo mapya yameongezeka katika ushiriki wa matembezi ya mwaka huu, kwa mara ya kwanza tutakuwa na Marathoni iliyokamilika ya kilomita 42.2.
  “Pia tutaongeza urefu wa mzunguko kwa waendesha baiskeli kotoka kilomita 21 hadi kilomita 42.2 na lengo kubwa la mbio na matembezi hayo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha afya cha CCBRT,” amesema Barrett.
  Naye Mkurugenzi wa Bank M, Jacqueline Woiso amesema kwamba wataendelea kutoa ushirikiano kwa Rotary Marathon kwa sababu wamekuwa wakishirikiana katika shuguli mbalimbali za kijamii na maendeleo kwa ujumla.
  Katika ushiriki wa mbio na matembezi hayo, watu wakubwa watalipia Sh. 35,000 na watoto Sh. 10,000 na utaratibu wa kununua fomu hizo utatangazwa kwenye vituo mbalimbali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MZEE RUKSA’ MGENI RASMI DAR MARATHON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top