• HABARI MPYA

    Wednesday, August 02, 2017

    YANGA ‘YATESTI MITAMBO’, YAWAPIGA MORO KIDS 5-0

    Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
    YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Moro Kids katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Seminari, Bigwa, Morogoro asubuhi ya leo. 
    Katika mchezo huo washambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma alifunga mabao mawili, Mrundi Amissi Tambwe moja na viungo Raphael Daudi na Yussuf Mhilu nao kila mmoja akafunga bao moja.
    Wachezaji wote waliopo kambini na Yanga katika hoteli ya B-Z eneo la Nane Nane mjini Morogoro walipewa nafasi ya kucheza mechi hiyo, kasoro kiungo mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa na winga mzawa, Geoffrey Mwashiuya ambao ni majeruhi.
    Amissi Tambwe amefunga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Moro Kida mjini Morogoro leo

    Baada ya mechi hiyo, Yanga inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumamosi wiki hii kucheza na Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga inatarajiwa na kumenyana na Singida United inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Mholanzi Hans van der Pluijm katika mchezo maalum wa kila timu kujaribu kikosi chake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Ikumbukwe Kikosi cha kocha Mzambia, George Lwandamina kipo kwenye maandalizi ya msimu mpya, ambao wataanza na mchezo wa Ngao ya Jamii, dhidi ya mahasimu, Simba, Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa.
    Singida United imerejea Ligi Kuu msimu huu tangu iliposhuka mwaka 2002, lakini baada ya kupanda imefanya usajili wa gharama kubwa, ikichukua wachezaji wenye uzoefu mkubwa kutokaa timu mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
    Maana yake si tu wanatarajiwa kutoa upinzani kwa Yanga Agosri 5, bali pia wanatarajiwa kuwa tishio katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA ‘YATESTI MITAMBO’, YAWAPIGA MORO KIDS 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top