• HABARI MPYA

  Thursday, January 08, 2015

  YANGA ‘OUT’ KOMBE LA MAPINDUZI, NI SIMBA NA POLISI, MTIBWA NA JKU NUSU FAINALI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  YANGA SC watapanda boti moja na Azam FC kesho kurejea Dar es Salaam kufuatia kutolewa katika Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi na JKU kwa kufungwa bao 1-0 usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Shukaa wa JKU, alikuwa ni mshambuliaji Amour Omar ‘Janja’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 72 kwa shuti kali lililomshinda kipa Ally Mustafa ‘Barthez’.
  Yanga SC leo hawakuwa na bahati, kwani vipindi vyote viwili walitengeneza nafasi nyingi nzuri za kufunga na wakaishia kukosa mabao ya wazi.
  Mshambuliaji wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman akikabiliana na beki wa JKU usiku Uwanja wa Amaan

  JKU ilitawala sehemu ya kiungo katika mchezo wa leo na Yanga SC ilipitisha mashambulizi mengi kupitia kwa mawinga hatari, Simon Msuva na Andrey Coutinho, lakini washambuliaji Amisi Tambwe na Kpah Sherman walishindwa kufunga. 
  JKU sasa itakutana na Mtibwa Sugar walioitoa Azam FC kwa penalti katika Nusu Fainali Jumamosi, wakati Simba SC itamenyana na Polisi iliyowatoa mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda.  
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua/Edward Charles dk81, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Amisi Tambwe/Mrisho Ngassa dk63, Kpah Sherman na Andrey Coutinho/Haruna Niyonzima dk51.
  JKU; Mohammed Abdulrahman, Pancian Malik, Abdallah Waziri, Khamis ABdallah, Issa Khaidary, Ismail Khamis, Isihaka Othman, Khamis Said, Amour Mohammed Janja, Hilal Rehani/Mbarouk Fakhi dk50 na Mohammed Abdallah/Salum Said dk62.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA ‘OUT’ KOMBE LA MAPINDUZI, NI SIMBA NA POLISI, MTIBWA NA JKU NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top