• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  YANGA NA AZAM HAZINA HABARI NA MECHI ZAO LEO, TFF YAACHIA HADI RATIBA HII HAPA!

  KICHEKESHO cha mwaka! Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa ratiba mpya ya Ligi Kuu, ikionyesha leo Yanga wananacheza na Coastal Union leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Azam FC na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Lakini ajabu, timu zote, Yanga na Azam hazina taarifa na mechi hizo na zote hazipo kwenye vituo vya michezo hiyo.
  Meneja wa Azam FC, Jemedari Said amesema wapo mkoani Shinyanga na wanajua mechi yao ni mwishoni mwa wiki.
  Kwa upande wake, Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh amesema timu yao ipo kambini Bagamoyo, inajiandaa na mechi na Ruvu Shooting Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA AZAM HAZINA HABARI NA MECHI ZAO LEO, TFF YAACHIA HADI RATIBA HII HAPA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top