• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  TFF YAAHIRISHA RASMI MECHI ZA YANGA NA AZAM FC

  MAZINGAOMBWE yanaendelea, saa kabla ya kuanza kwa mwchi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania leo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeahirisha mechi hizo.
  Mapema leo, BIN ZUBEIRY ilinasa nakala ya ratiba mpya ya Ligi Kuu, ikionyesha leo Yanga wananacheza na Coastal Union leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Azam FC na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Lakini BIN ZUBEIRY ilipowasiliana na timu zote, Yanga na Azam ajabu zilisema hazina taarifa na mechi hizo na zote hazipo kwenye vituo vya michezo hiyo.
  Meneja wa Azam FC, Jemedari Said amesema wapo mkoani Shinyanga na wanajua mechi yao ni mwishoni mwa wiki, wakati kwa upande wake, Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh amesema timu yao ipo kambini Bagamoyo, inajiandaa na mechi na Ruvu Shooting Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kufuatia BIN ZUBEIRY kuandika habari hizo, TFF imetangaza kuzifuta mechi hizo na kutoa ratiba nyingine tena, ambayo inasema mechi hizo zilizokuwa zichezwe leo, sasa zitatangazwa baadaye zitachezwa lini.
  Timu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu, Mtibwa Sugar, Azam FC, Yanga na Azam FC zilikwenda kucheza Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzabr na kila timu ikaahirishiwa mechi hizo mbili, ambazo inaonekana zinawasumbua kichwa TFF baada ya michuano hiyo kumalizika jana.  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAAHIRISHA RASMI MECHI ZA YANGA NA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top