// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WILDER AMTWANGA MHAITI NA KURUDISHA UFALME WA NDONDI ZA UZITO WA JUU MAREKANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WILDER AMTWANGA MHAITI NA KURUDISHA UFALME WA NDONDI ZA UZITO WA JUU MAREKANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, January 18, 2015

    WILDER AMTWANGA MHAITI NA KURUDISHA UFALME WA NDONDI ZA UZITO WA JUU MAREKANI

    BONDIA Mmarekani, Deontay Wilder amemuenzi vizuri bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani, Muhammad Ali baada ya Alfajiri ya leo kutawazwa kuwa bingwa wa dunia uzito wa juu.
    Hiyo inafuatia kumshinda Bermane Stiverne kwa pointi ukumbi wa MGM Grand mjini Las Vegas na kutwaa taji la WBC akiwa Mmarekani wa kwanza kushinda taji la uzito wa juu duniani baada ya miaka zaidi ya nane.
    Wilder, ambaye awali aliwakalisha ndani ya raundi ya tano wapinzani wake wote katika mapambano 32 yaliyopita, mara mbili alimpa kibano cha nguvu Stiverne, lakini hakufanikiwa kumpiga kwa Knockout mbabe huyo wa Haiti.
    Mwishowe akashinda pointi za majaji wote, 118-109, 119-108 na 120-107 dhidi ya Wilder. Ni ushindi ambao umekuja katika usiku ambao mbabe wa kihistoria kuwahi kutokea katika ndondi za uzito wa juu, Ali alikuwa anasherehekea miaka 73 ya kuzaliwa kwake.Stiverne fell to the canvas at the end of the second round but it was adjudged not to be a knockdown
    Stiverne akienda chini baada ya kibano cha Wilder, lakini alisimama na kuendelea na pambano
    Wilder unloaded with his right hand on several occasions but was unable to stop the stubborn Stiverne
    Wilder akimchapa Stiverne aliyeoonyesha usugu wa kukomaa na kumaliza pambano

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2915193/Deontay-Wilder-crowned-heavyweight-world-champion-points-win-Bermane-Stiverne.html#ixzz3P9YYvsde
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WILDER AMTWANGA MHAITI NA KURUDISHA UFALME WA NDONDI ZA UZITO WA JUU MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top