• HABARI MPYA

  Sunday, January 18, 2015

  KOPUNOVIC AWAAMBIA WACHEZAJI SIMBA SC HAKUNA KULALA HADI KIELEWEKE

  Na Juma Mohammed, MTWARA
  KOCHA mpya wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa jana ugenini, lakini amewaambia; “Hakuna kulala hadi kieleweke”.
  Mserbia huyo jana alishinda mechi ya sita mfululizo tangu aanze kazi mwezi huu, baada ya kuiongoza Simba SC kuilaza 2-0 Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  “Nimefurahi kwa ushindi huu wa ugenini, timu inaendelea kubadilika siku hadi siku, nawapongeza wachezaji wangu. Lakini hii ni ligi, unamaliza mchezo mmoja, unaingia kwenye maandalizi ya mchezo mwingine,”. 
  Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic amewataka wachezaji wake kutobweteka na ushindi wa jana

  “Kwa hivyo nawakumbusha wachezaji wangu kwamba, hatujamaliza kazi, tuelekeze nguvu zetu katika mechi ijayo,”alisema Kopunovic.
  Ushindi huo wa pili katika mechi tisa za Ligi Kuu kwa Simba SC msimu huu, unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi watimize pointi 12 na kufufua matumaini ya ubingwa. 
  Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Mganda, Dan Sserunkuma dakika ya 26 aliyemalizia kwa guu la kushoto kona ya Ramadhani Singano ‘Messi’. 
  Kipindi cha pili, Simba SC iliyotwaa Kombe la Mapinduzi Zanzibar wiki iliyopita chini ya Kopunovic, ilifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 68 kupitia kwa Elias Maguri aliyemalizia pasi ya Dan Sserunkuma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOPUNOVIC AWAAMBIA WACHEZAJI SIMBA SC HAKUNA KULALA HADI KIELEWEKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top