• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  WEST HAM YAING'OA KWA MATUTA EVERTON KOMBE LA FA

  TIMU ya West Ham United imeitoa kwa penalti 9-8 Everton katika mchezo wa marudio wa Raundi ya Tatu ya Kombe la FA usiku wa Jumanne Uwanja wa Upton Park, kufuatia sare ya 2-2. 
  Enner Valencia aliifungia bao la kwanza The Hammers dakika ya 56, kabla ya winga wa Toffees, Aiden McGeady kutolewa kwa kadi ya pili.
  Kevin Mirallas aliyetokea benchi, aliisawazishia Everton pungufu dakika ya 82 kabla ya Romelu Lukaku kufunga bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 97. Hata hivyo, mtokea benchi mwingine, Carlton Cole akaisawazishia West Ham dakika ya 113.
  Sifa zimuendee kipa wa Hammers, Adrian aliyefunga penalty ya mwisho na sasa West Ham watamenyana na Bristol City katika Raundi ya Nne wikiendi ya Januari 24 na 25.
  Kipa Adrian akishangilia baada ya kufunga penalti ya mwisho ya West Ham katika ushindi wa 9-8 dhidi ya Everton

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2908979/West-Ham-2-2-Everton-9-8-pens-Keeper-Adrian-scores-winner-penalty-shootout-snuff-10-men-Toffees-comeback-FA-Cup.html#ixzz3OkLmuRAE 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEST HAM YAING'OA KWA MATUTA EVERTON KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top