• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  WANAOTUBEZA SISI MABINGWA WA BONANZA, WASUBIRI MOTO WETU KWENYE LIGI- HANS POPPE

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wanaibeza timu yao kwamba ni mabingwa wa mashindano ya Bonanza, wasubiri kuona kazi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana baada ya Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Simba SC ikishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90, Hans Poppe alisema; “Wanatubeza sisi ni mabingwa wa mabonanza, wasubiri moto wetu katika Ligi,”.
  Hans Poppe (kulia) akiwa na Kombe la Mapinduzi jana Uwanja wa Amaan

  Simba SC haijashinda taji la Ligi Kuu kwa misimu miwili iliyopita, lakini imeweza kutwaa mataji matano madogo madogo katika kipindi hicho, ambayo ni Kombe la Saleh Hijja, BancABC, Mtani Jembe mara mbili na Kombe la Mapinduzi jana.
  Shujaa wa Simba SC alikuwa ni kipa Ivo Mapunda aliyetokea benchi dakika ya 90 kwenda kuchukua nafasi ya Peter Manyika na kuokoa penalti ya mwisho ya Mtibwa iliyopigwa na Vincent Barnabas.
  Awali, Ivo alishuhudia penalti ya Ibrahim Rajab ‘Jeba ikigonga mwamba wakati upande wa Simba SC, penalti ya Shaaban Kisiga ‘Malone’ ilipanguliwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed Kasarama.
  Penalti za Simba SC zilifungwa na Awadh Juma, Hassan Kessy, Hassan Isihaka na Dan Sserunkuma, wakati za Mtibwa zilifungwa na Aly Lundenga, Shaaban Nditi na Ramadhani Kichuya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WANAOTUBEZA SISI MABINGWA WA BONANZA, WASUBIRI MOTO WETU KWENYE LIGI- HANS POPPE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top