• HABARI MPYA

  Wednesday, January 07, 2015

  USAJILI WA KWANZA MAN UNITED DIRISHA DOGO HUU HAPA

  KLABU ya Manchester United imekubali kuingia Mkataba wa miezi 18 na kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes.
  Klabu hiyo inajiandaa kumtangaza rasmi kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 kusajiliwa kwake Old Trafford akasaidiane na David de Gea.
  Valdes amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Louis van Gaal kwa miezi miwili iliyopita akiwa mchezaji huru aliyetoka kupona majeruhi.
  Valdes was recovering from injury and has not played since last March
  Valdes amepona maumivu ya goti yaliyomuweka nje ya Uwanja tangu Machi mwaka jana

  Kocha wa United, Louis van Gaal hajazungumza mengi juu ya mipango yake kwa Valdes, lakini amevutiwa naye kiasi cha kutosha siku za karibuni kiasi cha kuridhia kumpa mkataba.
  Kuwasili kwa Valdes kutamoa De Gea ushindani wa kutosha  Old Trafford kwa mara ya kwanza. Kipa wa pili kwa sasa, Anders Lindegaard hana nafasi mbele ya Van Gaal. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: USAJILI WA KWANZA MAN UNITED DIRISHA DOGO HUU HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top