• HABARI MPYA

  Thursday, January 08, 2015

  UKISTAAJABU JEZI ZA TAIFA, BASI HUJAONA MAJI WANAYOKUNYWA!

  Mchezaji wa Taifa ya Jang'ombe akijimwagia maji kwa jagi baada ya kunywa katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi jana dhidi ya Simba SC Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Simba ilishinda 4-0.
  Nyota wa klabu ya Taifa iliyoaga Kombe la Mapinduzi jana akinywa maji ambayo yalichotwa kwenye ndoo ndogo waliyokuja nayo timu hiyo uwanjani 

  Hii ndiyo ya maji ambayo walikuwa wanakunywa kwa kupokezana kikombe wachezaji wa Taifa jana. Mtu anakunywa maji, kikombe kinatumbikizwa kwenye ndoo yanachotwa tena maji, anapewa mwingine. Sijui kiafya hii imekaaje!
  Hiki ni kikosi cha Taifa kilichomenyana na Simba jana, tazama kwa makini jezi, utagundua ni aina mbili tofauti.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UKISTAAJABU JEZI ZA TAIFA, BASI HUJAONA MAJI WANAYOKUNYWA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top