• HABARI MPYA

  Thursday, January 08, 2015

  KOCHA WA YANGA NA MPISHI WA BAO LA COUTINHO JUZI

  Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm (kulia) akipeana mikono na shabiki na mwanachama wa klabu hiyo, maarufu kama Carlos jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar wakati Simba SC ikimenyana na Taifa ya Jang'ombe katika Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi. Carlos alilala rumande juzi baada ya kuingia uwanjani na kwenda kuchukua glavu za akiba za kipa wa Shaba, Bakari Shaweji katika mchezo wa mwisho wa Kundi A, akidhani ni uchawi uliokuwa ukisababisha wachezaji wa timu yao wakose mabao ya wazi. Dakika tano baada ya Carlos kutoa glavu hizo, Yanga ilipata bao dakika ya 86 lililofungwa na Andrey Coutinho na Carlos akapewa sifa ya kusababisha bao hilo pekee katika ushindi wa 1-0.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA WA YANGA NA MPISHI WA BAO LA COUTINHO JUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top