• HABARI MPYA

  Friday, January 16, 2015

  TFF YAFUNGUKA ‘VURUGA VURUGA’ RATIBA LIGI KUU

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  RATIBA ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imeingizwa mechi za viporo zilizotokana na timu za Azam, Mtibwa Sugar na Simba kucheza michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 iliyomalizika wiki hii kisiwani Zanzibar.
  Vilevile mechi za viporo zimeingizwa kwa kuzingatia ushiriki wa timu za Azam kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Yanga kwenye Kombe la Shirikisho (CC) pamoja na mechi za kirafiki za Taifa Stars.
  Yanga itacheza na BDF ya Botswana kwenye mchezo utakaofanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa wakati Azam itaikabili El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex, Februari 15 mwaka huu.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi

  Mechi za viporo itakuwa kama ifuatavyo; Januari 20- Kagera Sugar na Azam (Mwanza), Januari 28- Simba na Mbeya City (Dar es Salaam), Februari 4- Coastal Union na Yanga (Tanga), Februari 11- Azam na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam) na Februari 11- Mgambo Shooting na Simba (Tanga).
  Februari 11- Yanga na Ndanda (Dar es Salaam), Februari 21- Mbeya City na Yanga (Mbeya), Februari 25- Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons (Morogoro), Februari 28- Simba na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam), Machi 4- Ruvu Shooting na Azam (Pwani), na Machi 4- JKT Ruvu na Yanga (Dar es Salaam).
  Machi 4- Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro (Morogoro), Machi 8- Simba na Yanga (Dar es Salaam), Machi 11 Azam na Mbeya City (Dar es Salaam), Machi 11- Yanga na Kagera Sugar (Dar es Salaam), Machi 18- Azam na Ndanda (Dar es Salaam), Machi 18- Yanga na Stand United (Dar es Salaam), Aprili 8- Simba na Tanzania Prisons (Dar es Salaam).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAFUNGUKA ‘VURUGA VURUGA’ RATIBA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top