• HABARI MPYA

  Friday, January 16, 2015

  AMAVUBI KUTUA MWANZA JANUARI 21

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) inawasili Mwanza, Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
  Amavubi yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya JB Belmont.
  Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaingia kambini keshokutwa (Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata itakwenda Mwanza tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.
  Kikosi hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kinaundwa na wachezaji 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMAVUBI KUTUA MWANZA JANUARI 21 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top