• HABARI MPYA

  Friday, January 16, 2015

  NDANDA YAJIFICHA MAFICHONI KUMUWINDA MNYAMA JUMAMOSI

  Na Juma Mohammed, MTWARA
  BAADA ya kutoa sare na Polisi Moro Uwanja wa nyumbani, Ndanda FC sasa imepiga kambi katika mji mdogo wa Ndanda kuwawinda Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaochezwa kesho.
  Timu hiyo ambayo kwa sasa imepoteza imani kwa mashabiki wake ipo katika maandalizi mazito ili kuhakikisha inawazamisha mabingwa mara tatu wa Kombe Mapinduzi ili kurejesha imani kwa mashabiki wake,
  Siku za hivi karibuni mashabiki wa timu hiyo walilalamikia uongozi wa timu hiyo kufanya kambi Dar lakini mwenyekiti wa timu hiyo Ahmad Omary alifafanua kuwa wamekuwa dar kwa muda mrefu kwa kuwa ni rahisi kupata mechi za kirafiki na timu kubwa kuliko mtwara
  Ingawa uongozi wa Ndanda umekuwa hauko wazi kuhusu wapi ilipo timu hiyo lakini jitihada za mwandishi wa mtandao huu zimebaini kuwa timu hiyo imerudi Ndanda nje  ya mji wa mtwara kupitia mmoja wa wachzaji wa timu hiyo
  "Tupo Ndanda tumepiga kambi huku ila tutarudi mjini muda wowote" kilisema chanzo hicho"
  Awali timu za Ndanda na Simba zilikutana  katika mchezo wa kirafiki uliochezwa nangwanda sijaona kwenye maadhimisho ya NDANDA DAY ambapo timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDANDA YAJIFICHA MAFICHONI KUMUWINDA MNYAMA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top