• HABARI MPYA

  Sunday, January 04, 2015

  ‘STRAIKA LA AZAM’ LAITWA KIKOSI CHA MALI MATAIFA YA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, BAMAKO
  MSHAMBULIAJI ambaye Azam FC walitaka kumsajili Desemba, Mohamed Traore (pichani juu) wa El Merreikh ya Sudan ameitwa kwenye kikosi cha Mali kitakachocheza Fainali za Mataifa ya Afrika.
  Traore ameitwa kufuatia mshambuliaji wa FC Girondins de Bordeaux ya Ufaransa, Cheick Diabate, kuumia na kuenguliwa kwenye kikosi hicho.
  Mshambuliaji huyo tegemeo wa Mali mwenye umri wa miaka 26, atakuwa nje kwa miezi minne baada ya kuumia goti na anatarajiwa kwenda kufanyiwa upasuaji kwa mujibu wa klabu yake inayoshiriki Ligue 1.
  Diabate ameifungia mabao manane Bordeaux katika Ligi ya Ufaransa baada ya kucheza mechi 15, huku pia akitoa pasi mbili za mabao.
  Traore aliwekwa katika orodha ya wahezaji wa akiba wakati Mali inataja kikosi chake cha mwisho na sasa atalazimika kuiacha kambi ya Merreikh nchini Qatar ili kujiunga na timu yake ya taifa kwa maandalizi ya AFCON.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘STRAIKA LA AZAM’ LAITWA KIKOSI CHA MALI MATAIFA YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top