• HABARI MPYA

  Sunday, January 04, 2015

  KASHI AITWA KUZIBA PENGO LA ABEID ALGERIA

  Na Mwandishi Wetu, ALGIERS
  KIUNGO Ahmed Kashi (pichani juu) ambaye hajawahi kuichezea hata mechi moja Algeria, ameitwa kwenye kikosi cha Fainali za Mataifa ya Afrika.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mzaliwa wa Ufaransa anayechezea FC Metz ameitwa kwenda kuziba pengo la majeruhi Medhi Abeid wa Newcastle United. 
  Taarifa hizo zimevunja kwenye vyombo vya habari Algeria, ingawa Shirikisho la Soka la nchi hiyo bado halijathibitisha.
  Algeria walikuwa wa kwanza kati ya nchi 16 zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo kutaja kikosi chao cha mwisho, lakini bado wana wiki ya kufanya marekebisho kabla ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KASHI AITWA KUZIBA PENGO LA ABEID ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top