• HABARI MPYA

  Sunday, January 04, 2015

  EQUATORIAL GUINEA YAFUKUZA KOCHA BAADA YA KUPIGWA NA KITIMU CHA DARAJA LA NNE

  Na Mwandishi Wetu, BATA
  WENYEJI wa Fainal za Mataifa ya Afrika, Equatorial Guinea wamemfukuza kocha wao, Andoni Goikoetxea (pichani kulia) kiasi cha wiki tatu kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
  Goikoetxea aliondoka Alhamisi baada ya uchaguzi wa Rais mpya wa Shirikisho la Soka Equatorial Guinea (FEGUIFUT) wiki iliyopita.
  Rais mpya wa FEGUIFUT, Andres Jorge Mbomio amethibitisha kufukuzwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania, ambaye amekuwa kazini kwa miaka miwili iliyopita. Lakini hakutoa sababu za kufikia uamuzi huo.
  Bila shaka, kushindwa kwa timu hiyo kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kabla ya zali la Equatorial Guinea kupewa uenyeji, pamoja na kufungwa katika mechi mbili za kirafiki nchini Ureno zinaweza kuwa zimechangia kutimuliwa kwake.
  Equatorial Guinea, waliopewa uenyeji wa AFCON baada ya Morocco kujitoa, wamekuwa kwenye kambi ya maandalizi Ureno, lakini wamefungwa na timu ya Daraja la Nne, Villafranquense na timu B ya Benfica.
  Wenyeji hao watacheza na Kongo katika mchezo wa kwanza mjini Bata Januari 17 kwenye michuano hiyo inayoshirikisha timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EQUATORIAL GUINEA YAFUKUZA KOCHA BAADA YA KUPIGWA NA KITIMU CHA DARAJA LA NNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top