TIMU ya Manchester City imeifikia kwa pointi Chelsea kileleni mwa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sunderland Uwanja wa Etihad.
Shukrani kwake, kiungo mkongwe Frank Lampard aliyeifungia City bao la ushindi dakika ya 73 kwa kichwa akimalizia krosi ya Gael Clichy na timu hiyo inatimiza pointi 46 na mechi moja zaidi ya The Blues, 20.
Baada ya kipindi cha kwanza kibovu, City iliingia na moto kipindi cha pili wakati Yaya Toure alipoifungia bao la kwanza nje ya boksi dakika ya 56, kabla ya Stevan Jovetic kufunga la pili dakika ya 66.
Sunderland ikafanikiwa kusawazisha mabao yote akianza Jack Rodwell dakika ya 68 akiifunga klabu yake ya zamani na Adam Johnson kwa penalty dakika ya 72 baada ya Pablo Zabaleta kumchezea rafu Billy Jones.
Frank Lampard akionyesha dole gumba baada ya kuifungia Man City bao la ushindi
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2893373/Manchester-City-3-2-Sunderland-Frank-Lampard-scores-winner-settle-thrilling-contest-Manuel-Pellegrini-s-men-draw-level-points-Chelsea-Premier-League.html#ixzz3NaudrYSf
0 comments:
Post a Comment