• HABARI MPYA

  Saturday, January 17, 2015

  SIMBA SC YA GORAN IPITIE MBALI, NDANDA AFA 2-0 NANGWANDA

  Na Juma Mohammed, MTWARA
  KOCHA mpya wa Simba SC, Goran Kopunovic raia wa Serbia ameendeleza wimbi la ushindi katika mechi ya sita mfululizo, baada ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara jioni ya leo.
  Ushindi huo wa pili katika mechi tisa za Ligi Kuu kwa Simba SC msimu huu, unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi watimize pointi 12 na kufufua matumaini ya ubingwa. 

  Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Mganda, Dan Sserunkuma dakika ya 26 aliyemalizia kwa guu la kushoto kona ya Ramadhani Singano ‘Messi’. 
  Kipindi cha pili, Simba SC iliyotwaa Kombe la Mapinduzi Zanzibar wiki iliyopita chini ya Kopunovic, ilifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 68 kupitia kwa Elias Maguri aliyemalizia pasi ya Dan Sserunkuma.
  Kikosi cha Ndanda FC kilikuwa; Saleh Malande, Aziz Sibo, Paul Ngalema, Cassian Ponella, Ernest Mwalupani, Zabron Raymond, Stamil Mbonde, Omega Seme, Omary Nyenje/Said Issa dk62, Gideon Benson/Salum Mineli dk80 na Jacob Massawe/Masoud Ali dk77.
  Simba SC; Peter Manyika, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/Awadh Juma dk80, Said Ndemla, Dan Sserunkuma/Abdi Banda dk85, Elias Maguli na Emmanuel Okwi.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YA GORAN IPITIE MBALI, NDANDA AFA 2-0 NANGWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top