GWIJI wa masumbwi duniani, Muhammad Ali ameruhusiwa kutoka hospitali nchini Marekani ambako alikuw amelazwa kwa matibabu ya kibofu cha mkojo na leo atasherehekea kuzaliwa kwake pamoja na familia.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa bondia huyo kulazwa hospitali katika wiki nne zilizopita.
Msemaji wa familia ya Ali, Bob Gunnell amesema aliondoka katika hospitali ambayo haikutajwa na kurejea katika moja ya nyumba zake.
Muhammad Ali ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya matibabu ya kibofu cha mkojo
Ali, akiwa amesimama baada ya kumbwaga chini Sonny Liston mwaka 1965, anapewa heshima ya bondia bora wa uzito wa juu daima
Gunnell amesema Ali anatarajiwa kusherehekea miaka ya 73 ya kuzaliwa kwake na familia pamoja marafiki na jamaa mbalimbali.Bingwa huyo wa ndondi za uzito wa juu wa zamani duniani na mkewe, Lonnie, wana nyumba Arizona, Michigan na nyumbani kwao, Louisville.
Ali alipeleka hospitali mwishoni mwa mwezi uliopita kwa maradhi ambayo awali ilidhaniwa ni Nimonia. Baadaye madaktari wakagundua Ali anasumbuliwa na matatizo ya kibofu cha mkojo na si Nimonia.
0 comments:
Post a Comment