• HABARI MPYA

  Tuesday, January 13, 2015

  SIMBA SC HATARINI KUMKOSA SIMON SSERUNKUMA LEO DHIDI YA MTIBWA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  SIMBA SC iko hatarini kumkosa mshambuliaji wake, Simon wake Sserunkuma katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mganda huyo jana alikuwa nje wakati wenzake wanafanya mazoezi Uwanja wa Chukwani, kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Polisi Jumamosi, Simba SC ikishinda 1-0.
  Sserunkuma aliyesajiliwa Desemba kutoka Express ‘Tai Wekundu’ ya Kampala alikwatuliwa mara kadhaa na mabeki wa Polisi Jumamosi kabla ya kupumzishwa dakika ya 79 kumpisha Awadh Juma.
  Mshambuliaji wa Simba SC, Simon Sserunkuma hakufanya mazoezi jana kwa sababu ya maumivu ya kifundo cha mguu

  Lakini alitoka akiwa tayari ameisetia Simba SC bao pekee la ushindi dakika ya 26 lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ kwa mpira wa adhabu baada ya Mganda huyo kuangushwa pembezoni mwa Uwanja kulia.
  Kocha wa Wekundu wa Msimbazi, Mserbia Goran Kopunovic amesema jana kwamba hawezi kumtumia mchezaji huyo akiwa ana maumivu kwa sababu italeta athari kubwa.
  “Lengo langu kubwa ni Ligi Kuu, lazima niende kwenye Ligi nina wachezaji wa kutosha na walio fiti, kama nitazungumza na Simon asubuhi (leo), akisema hasikii maumivu, naweza kumtumia, vinginevyo hatacheza,”amesema.
  Kocha Goran Kopunovic (kulia) aliongoza mazoezi Simba SC jana bila SImon Sserunkuma

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC HATARINI KUMKOSA SIMON SSERUNKUMA LEO DHIDI YA MTIBWA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top