• HABARI MPYA

  Saturday, January 03, 2015

  SHERMAN: SASA NI MABAO TU YANGA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  MSHAMBULIAJI Mliberia wa Yanga SC, Kpah Sean Sherman amesema kwamba alikuwa anasubiri sana kufunga bao lake la kwanza katika klabu hiyo na sasa ni wakati wa kukuza akaunti yake mabao Jangwani.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya mchezo wa Kombe la Mapinduzi jana dhidi ya Taifa ya Jang’ombe Uwanja wa Amaan mjini hapa jana, Sherman alisema kwamba amefurahi kufunga katika ushindi wa 4-0.
  “Nilisubiri sana kufunga bao langu la kwanza hapa, sikuweza kufunga katika mechi ya kwanza na ya pili. Na leo (jana) kipindi cha kwanza nimekosa mabao mawili ambayo sikuamini.
  Kpah Sean Sherman amefurahia kufunga bao lake la kwanza jana Yanga SC

  Nilikwenda chumba cha kubadilishia nguo nikiwa mnyonge sana, lakini nashukuru kocha akaniacha niendelee na hatimaye nimefunga bao langu la kwanza hapa. Nimefurahi, sasa nataka kukuza akaunti yangu ya mabao Yanga,”amesema.  
  Mbali na kufunga bao hilo, Sherman pia alimsetia Simon Msuva kufunga bao la kwanza katika mabao yake matatu jana mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi.
  Mshambuliaji huyo aliyekuwa anacheza Cyprus Kaskazini, alitua Yanga SC mwezi uliopita na hadi sasa amekwishacheza mechi tatu, ya kwanza wakifungwa 2-0 na Simba katika Nani Mtani Jembe na baadaye katika sare ya 2-2 na Azam FC Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHERMAN: SASA NI MABAO TU YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top