• HABARI MPYA

  Saturday, January 03, 2015

  SABABU KWA NINI KIPRE TCHETCHE, KAVUMBANGU HAWAKUWEPO HATA BENCHI JANA

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  WASHAMBULIAJI tegemeo wa Azam FC, Mrundi Didier Kavumbangu na Kipre Herman Tchetche hawakuichezea Azam FC jana dhidi ya KCCA ya Uganda kwa sababu wagonjwa.
  Azam FC ililazimishwa sare ya 2-2 na mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, KCCA katika mchezo wa Kundi B michuano hiyo Uwanja wa Amaan wakati wawili hao hawakuwepo hata benchi.
  Kwa kuwa walicheza mechi iliyopita dhidi ya Yanga SC timu hizo zikitoka sare ya 2-2 katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja a Taifa, Dar es Salaam, kukosekana kwao jana kulizua minong’ono.
  Didier Kavumbangu anasumbuliwa na homa ndiyo sababu hakucheza jana
  Kipre Tchetche ana maumivu ya kifundo cha mguu ndiyo maana hakucheza jana

  Hata hivyo, kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Marius Omog raia wa Cameroon amesema wapachika mabao wake tegemeo hao wote ni wagonjwa.
  Omog alisema Kipre Tchetche alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu, wakati Kavumbangu ana homa.
  “Hawako vizuri wote, wanaumwa. Kipre anasumbuliwa enka na Kavumbangu ana homa kidogo,”alisema Omog.
  Kuhusu kumuacha benchi beki wa Ivory Coast, Serge Wawa Pascal aliyesajiliwa kutoka El Merreikh ya Sudan Desemba, Omog alisema; “Nilitaka kuona wachezaji wengine”.
  Jana Omog aliwaanzisha David Mwantika na Aggrey Morris katika beki ya kati, Wawa na Mourad wakibaki benchi.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SABABU KWA NINI KIPRE TCHETCHE, KAVUMBANGU HAWAKUWEPO HATA BENCHI JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top