• HABARI MPYA

  Monday, January 05, 2015

  REAL MADRID YACHAPWA 2-1 LA LIGA

  REAL Madrid wameangukia pua Uwanja wa Mestalla, baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji Valencia katika mchezo wa la Liga usiku huu.
  Kipigo hicho kinaamanisha wimbi la ushindi la Real Madrid katika mechi 22 mfululizo limezimwa na Valencia. Cristiano Ronaldo alitangulia kuifungia Real kwa penalti dakika ya 14 tu ya mchezo huo, baada ya Alvaro Negredo kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
  Beki wa Valencia, Antonio Barragan Fernandez akaisawazishia timu yake dakika ya 52, kabla ya Nicolas Otamendi kufunga la ushindi dakika ya 65 kwa kichwa akimalizia kona ya Daniel Parejo.
  Kikosi cha Valencia kilikuwa; Diego Alves, Barragan/Feghouli dk73, Otamendi, Mustafi, Orban, Parejo, Enzo Perez, Andre Gomes, Piatti/Gaya dk23, Negredo/Rodrigo dk80 na Alcacer.
  Real Madrid: Casillas, Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo, Isco, Kroos, James/Khedira dk71, Bale/Jese dk71, Benzema/Hernandez dk80 na Ronaldo.
  Real Madrid record signing Bale (left) is tackled by Valencia's Lucas Orban to concede a first-half free kick
  Mchezaji ghali wa Real Madrid, Gareth Bale (kushoto) akidhibitiwa na beki wa Valencia, Lucas Orban katika mchezo huo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2896362/Valencia-2-1-Real-Madrid-Cristiano-Ronaldo-hits-spot-Los-Blancos-22-game-winning-streak-comes-end.html#ixzz3NtXDPB9B 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YACHAPWA 2-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top