• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  RAIS SHEIN AMPONGEZA MANYIKA, AMUAMBIA AONGEZE BIDII ATISHE ZAIDI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein jana alimpongeza kipa wa Simba SC, Peter Manyika na kumtaka aongeze juhudi aje kuwa bora zaidi baadaye.
  Rais Shein alimpa pongezi hizo Manyika wakati anamvisha Medali ya ushindi wa Kombe la Mapinduzi kufuatia kuifunga Mtibwa Sugar kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  “Rais amenipongeza wakati ananivalisha Medali, akaniambia niongeze juhudi nije kuwa kipa bora zaidi,”alisema Manyika jana baada ya kuulizwa na BIN ZUBEIRY aliambiwa nini Rais Shein wakati anavalishwa Medali. 
  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein aliteta na Peter Manyika wakati anamvalisha Medali jana Uwanja wa Amaan
  Manyika amefungwa bao moja tu katika mechi zote sita za Kombe la Mapinduzi alizodaka hadi Simba inatwaa ubingwa jana

  Manyika alidaka kwa dakika 90 na ushei jana bila kufungwa kabla ya kumpisha Ivo Mapunda aliyemalizia vizuri mchezo kwa kuokoa penalti na Simba SC ikatwaa Kombe. 
  Manyika amedaka mechi zote za Simba SC Kombe la Mapinduzi kuanzia hatua ya makundi na kufungwa bao moja tu katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar, Wekundu wa Msimbazi wakilala 1-0.
  Angeweza kutangazwa kipa bora jana, kama Simba SC ingechomoza na ushindi ndani ya dakika 90, lakini akazidiwa kete na Said Mohamed wa Mtibwa aliyecheza penalti moja katika matuta.
  Mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga SC, wengi wanamtabiria kuwa mlinda mlango tegemeo la taifa baadaye iwapo ataongeza bidii. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS SHEIN AMPONGEZA MANYIKA, AMUAMBIA AONGEZE BIDII ATISHE ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top