// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOPUNOVIC: LIGI KUU NDIYO MUHIMU ZAIDI KWANGU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOPUNOVIC: LIGI KUU NDIYO MUHIMU ZAIDI KWANGU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, January 14, 2015

    KOPUNOVIC: LIGI KUU NDIYO MUHIMU ZAIDI KWANGU

    Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
    KOCHA wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic amewapongeza wachezaji kwa ushindi wa Kombe la Mapinduzi jana, lakini amewataka wasibweteke, kwani Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ndiyo mashindano muhimu zaidi kwake. 
    “Nimefurahi sana kutwaa Kombe hili, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi nzuri, ni jambo la kujivunia kuanza vizuri, kumbuka nina wiki ya pili tu tangu nisaini Mkataba, nimefurahi sana,”alisema kocha huyo wa zamani wa Polisi ya Rwanda.
    Hata hivyo, Mserbia huyo amewaambia wachezaji wake kwamba hawatakiwi kubweteka na ushindi huo, badala yake wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika Ligi Kuu, ambayo ni muhimu zaidi.
    Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic (kulia) akiwa ameshika kwa pamoja Kombe la Mapinduzi na Msaidizi wake, Suleiman Matola jana Uwanja wa Amaan

    “Kwangu mimi muhimu zaidi ni Ligi Kuu, pamoja na kuwapa pongezi vijana wangu, lakini nawaambia tunatakiwa kufanya kazi ngumu zaidi katika Ligi, kwangu mimi Ligi Kuu ndiyo kitu muhimu zaidi,”amesema.    
    Mchezo wa jana ulikuwa wa tano mfululizo Simba SC inashinda chini ya Goran, ambaye sasa anaipiku rekodi ya kocha aliyemtangulia, Mzambia Patrick Phiri aliyeshinda mechi nne mfululizo za awali.
    Phiri aliyeanza kazi Agosti mwaka jana Simba SC akimpokea Mcroatia, Zdravko Logarusic alishinda mechi nne mfululizo za kirafiki mwanzoni, kabla ya kufungwa mechi ya tano na tangu hapo, timu ikawa inasuasua hadi akafukuzwa kazi Desemba mwishoni.
    Phiri alishinda 2-1 dhidi ya Kilimani City, 2-0 dhidi ya Mafunzo na 5-0 dhidi ya KMKM, zote za kirarfiki Uwanja wa Amaan, Zanziabr na baadaye 3-0 dhidi ya Gor Mahia kirafiki pia, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hata hivyo, katika mchezo wa tano ambao ulikuwa wa kirafiki pia, Phiri alifungwa 1-0 na URA Dar es Salaam na huo ukawa mwisho wa rekodi yake ya wimbi la ushindi wa mechi nne.
    Goran aliyeanza kazi Janauri, pia mechi za mwanzo amecheza Zanzibar na hadi sasa ameshinda tano mfululizo dhidi ya Mafunzo 1-0, JKU 1-0, Taifa Jang’ombe 4-0 na Polisi 1-0 pia na jana dhidi ya Mtibwa Sugar akibeba na Kombe la Mapinduzi.
    Simba SC ilipoteza mechi ya kwanza ya mashindano kwa kufungwa 1-0 na Mtibwa Sugar, lakini wakati huo Kopunovic alikuwa hajaanza kazi na timu ilikuwa chini ya kocha Msaidizi, Suleiman Matola. 
    Ikumbukwe, Phiri hakuweza kuvunja rekodi ya Logarusic, aliyeshinda mechi tano mfululizo tangu arithi mikoba ya Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ Desemba mwaka juzi.
    Loga alizifunga KMKM 3-1 kirafiki, Yanga SC 3-1 pia Nani Mtani Jembe, KMKM tena 1-0 Kombe la Mapinduzi, Chuoni 2-0, URA 2-0 kabla ya kukwama kwa KCC katika Fainali Kombe la Mapinduzi akifungwa 1-0.
    Hata hivyo, kwa miaka ya karibuni, chini ya makocha tofauti, Simba SC imekuwa tishio katika mashindano ya vikombe vidogo vidogo, lakini inapowadia Ligi Kuu makali yao hupotea kitu ambacho Goran anataka kubadilsiha.
    Ataanza Ligi Kuu kwa kuiongoza Simba SC katika mchezo wa ugenini dhidi ya Ndanda FC Janauri 17, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
    Baada ya hapo ataifuata Mgambo Shooting mjini Tanga katikati ya wiki na mwishoni mwa wiki,  Januari 24 atakutana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Simba SC kabla ya kumalizia kiporo katikati ya wiki na Mbeya City Dar es Salaam.
    Wazi mechi hizo nne ndiyo zitatoa taswira ya mustakabali wa Mserbia huyo Msimbazi, ambaye amepewa Mkataba wa awali wa majaribio wa miezi sita.
    Simba SC imekubaliana na Kopunovic, iwapo atafanya vizuri katika sehemu iliyobaki ya msimu, ataongezewa Mkataba wa miaka miwili, lakini akichemsha ataonyeshwa mlango waliotokea Mserbia mwenzake Milovan Cirkovic, Mfaransa Patrick Liewig, mzalendo Kibadeni, Logarusic na Phiri ndani ya miaka miwili iliyopita.
    Phiri aliondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi nane, akishinda moja, kufungwa moja na sare sita, hivyo kukusanya pointi tisa, ikizidiwa pointi saba na Mtibwa Sugar walio kileleni. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOPUNOVIC: LIGI KUU NDIYO MUHIMU ZAIDI KWANGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top