• HABARI MPYA

  Sunday, January 18, 2015

  OMOG: MOTO HUU HADI UBINGWA

  Na Philipo Chimi, SHINYANGA
  KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog amesema timu yake itaendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa lengo la kutetea ubingwa.
  Watetezi hao wa taji, Azam FC jana walishinda bao 1-0 dhidi ya wenyeji Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Shukrani kwake, kiungo aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, Frank Raymond Domayo aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 43 na sasa Azam FC inatimiza pointi 17 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi kwa pointi moja Mtibwa Sugar iliyokuwa juu kwa muda mrefu. 
  Kikosi cha Azam FC kilichoifunga Stand United 1-0 jana

  “Nimefurahishwa na matokeo haya, mchezo ulikuwa mgumu, wapinzani wetu ni wazuri, lakini tutaendelea kupambana tuendeleze wimbi la ushindi kwa lengo la kutetea ubingwa,”alisema Omog baada ya mechi. 
  Kwa upande wake, Kocha Msaidiziwa Stand, Emmanuel Massawe akiuzungumzia mchezo huo, alisema bahati haikuwa yao, kwani walitengeneza nafasi wakashindwa kutumia.
  Massawe amesema sasa wanaelekeza nguvu zao katika mchezo ujao dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
  Azam FC sasa, sasa inaelekea Mwanza, ambako Jumanne itamenyana na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG: MOTO HUU HADI UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top