• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  OKWI: MCHEZO ULINIKATAA, INATOKEA

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  MSHAMBULIAJI Mganda wa Simba SC, Emmanuel Okwi amesema jana hakucheza vizuri dhidi ya Mtibwa Sugar na hiyo ni hali ya kawaida inayoweza kumtokea mchezaji yeyote.
  Simba SC ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 dhidi ya Mtibwa Sugar jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar na kutwaa Kombe la Mapinduzi.
  Na kocha Mserbia, Goran Kopunovic alimtoa Okwi uwanjani dakika ya 75 kumpisha kiungo Awadh Juma Issa ‘Mtani Jembe’ baada ya kushindwa kuonyesha cheche.
  Emmanuel Okwi akiwa na Kombe la Mapinduzi jana
  Okwi (kushoto) akiwania mpira dhidi ya Ally Shomary wa Mtibwa jana 

  “Kweli, sikucheza vizuri, ni hali ambayo inaweza kumtokea mchezaji yeyote duniani, kuna wakati mchezo unamkataa. Mimi leo (jana) mchezo umenikataa, ila bado ni Okwi yule yule na watu wasubiri kuniona mechi zijazo,”amesema.
  Wengi wanaamini kutokuwa kambini kwa takriban wiki mbili akiwa kwao, Uganda kwa ajili ya shughuli za ndoa yake ndiyo kulimfanya Okwi acheze chini ya kiwango chake jana, lakini mwenyewe anasistiza ni hali ya kawaida ya mchezo.
  “Mimi nilipokuwa Uganda nilikuwa nafanya mazoezi siku zote, na nimekuja hapa nimefanya mazoezi na timu siku tatu, ingetosha kabisa kunifanya nicheze kama kawaida yangu. Ila mchezo umenikataa,”amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI: MCHEZO ULINIKATAA, INATOKEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top