• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  NDEMLA HATARINI KUWAKOSA NDANDA JUMAMOSI

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  KIUNGO Said Hamisi Ndemla yuko hatarini kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara mwishoni mwa wiki, baada ya kuumia nyama jana.
  Ndemla alitolewa dakika ya 89 jana na nafasi yake kuingia mkongwe Shaaban Kisiga ‘Malone’ baada ya kuumia nyama katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mchezo huo, uliohudhuriwa na Rais wa Zanzibar Dk, Ali Mohammed Shein uliisha kwa sare ya bila kufungana na Simba SC ikashinda kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90.
  Said Ndemla akisindikizwa kwenye benchi jana na Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe

  Ndemla aliiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba ameumia nyama na atasikilizia hali yake siku mbili zijazo ili kujua uzito wa maumivu yake.
  “Nimeumia nyama, sasa sijui itakuwa ni maumivu makubwa kiasi gani, nadhani nitajua baada ya siku mbili au tatu,”alisema Ndemla, ambaye ameng’ara kwenye Kombe la Mapinduzi. 
  Simba SC watakuwa wageni wa Ndanda Uwanja wa Nangwanda, Sijaona mjini Mtwara Jumamosi katika mfululizo wa Ligi Kuu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDEMLA HATARINI KUWAKOSA NDANDA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top