• HABARI MPYA

  Saturday, January 03, 2015

  NDEMLA AING’ARISHA SIMBA SC ZANZIBAR

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  BAO pekee la kiungo Said Hamisi Ndemla limeipa ushindi wa 1-0 Simba SC katika mchezo wa Kundi C Kombe la Mapinduzi jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Ushindi huo katika mechi ya kwanza chini ya kocha mpya, Mserbia Goran Kopunovic unakuwa faraja kwa kwa wana Simba SC, baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa 1-0 na Mtibwa Sugar juzi.
  Katika mchezo wa leo, Simba SC ililalizimika kusubiri hadi kipindi cha pili kupata ushindi huo, baada ya Ndemla kufumua shuti kali la umbali wa mita takriban 30 kufuatia pasi ya Hassan Ramadhani Kessy dakika ya 54.
  Katika mchezo mwingine wa kundi hilo uliotangulia leo, Mtibwa Sugar ililalizimishwa sare ya 1-1 na JKU. 
  Said Ndemla (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao pekee Simba SC leo Uwanja wa Amaan

  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi nne, Saa 9:00 Alasiri, mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda wakimenyana na Mtende Uwanja wa Amaan wakati huo huo Taifa Jang’ombe wakipepetana na Shaba Uwanja wa Mao dze Tung.
  Uwanja wa Amaan, Saa 11:00 jioni Yanga SC watamenyana na Polisi kabla ya mabingwa wa Zanzibar, KMKM kumenyana na mabingwa Bara, Azam FC Saa 2:15 usiku. 
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdul Banda, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/Twaha Ibrahim ‘Messi’ dk72, Said Ndemla, Dan Sserunkuma/Ibrahim Hajibu dk80, Elias Maguri na Awadh Juma.
  Mafunzo; Hashim Haroun, Hajji Abdi, Abdulhalim Abdallah, Said Mussa, Juma Othman, Hassan Ahmad/Wahid Ibrahim dk77, Ali Othman/Amour Abdallah dk84, Ali Mbarouk, Sadik Habib/Rashid Abdallah dk47, Mohamed Abdulrahim na Ali Juma.
  Kiungo wa Mafunzo Ali Mbarouk akimdhibiti mshambuliaji wa Simba, Dan Sserunkuma. Kulia ni beki Juma Othman Mmanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDEMLA AING’ARISHA SIMBA SC ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top