• HABARI MPYA

  Friday, January 16, 2015

  31 WAITWA KAMBI YA U23 KENYA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  Shirikisho la Soka la Kenya, FKF, imetoa orodha ya kikosi cha wachezaji 31 wasiozidi umri wa miaka 23 kitakachowakilisha Kenya katika michuano ya kufuzu kushiriki Mechi za bara Afrika (All Africa Games) na mashindano ya Afrika kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 23.
  Kikosi hicho kitakacho ongozwa na kocha wa timu ya taifa Harambee Stars na Msikochi Bobby Williamson kinajumuisha wachezaji 28 wanaocheza ligi kuu ya Kenya huku watatu tu wakitoka ligi za chini.
  Kenya itaanza kampeni yake dhidi ya Misri (All Africa Games) ugenini kati ya tarehe 21 – 22 Februari huku mkumbo wa pili ukisakatwa majuma mawili baadaye.
  Ismael Dunga wa Tusker amejumuishwa kikosini

  Mshindi atamenyana na aidha Burundi ama DR Congo katika awamu ya pili mwezi Aprili 2015.
  Katika michuano ya vijana wasiozidi miaka 23, Kenya watakuwa ugenini dhidi ya Botswana tarehe 24 ama 25 Aprili kisha marudiano kati ya tarehe 8 au 9 Mei, atakayeibuka na ushindi atapapurana na Ivory Coast.
  Kikosi hicho kinachomujumuisha kiungo wa AFC Leopards Timonah Wanyonyi kitaingia kambini siku ya Jumatatu, 19 Januari uwanjani Kasarani.
  WALINDALANGO: Ian Otieno (Posta Rangers), Bonface Baraza (Intercity), Eliud Emase (West Kenya), Robert Mboya (Mathare United) 
  MABEKI: Collins Shivachi (Sofapaka), Sosthenes Idah FC (KCB), Sammy Meja (Thika United), Aboud Omar (Tusker FC), Charles Odette (Posta Rangers), Vincent Omumbo (Thika United), Robinson Mwangi Kamura (Mathare United), Bernard Odhiambo (Gor Mahia), Bryan Birgen (Ulinzi Stars).
  VIUNGO: John Ndirangu (Bandari FC), Joseph Wanyonyi (AFC Leopards), Titus Achesa (Shabana FC), Victor Ndinya (Bandari), Victor Ashinga (Nairobi City Stars), Vincent Odongo (Mathare United), Anthony Mbugua (Liberty Sports Academy), David King’atua (Thika United), Tairus Omondi (KCB FC), Michael Mutinda Kyalo (Thika United), Stephen Wakanya (Chemelil Sugar).
  WASHAMBULIZI: Agwanda Enock (Sofapaka FC), Michael Olunga (Gor Mahia), Meshack Karani (Chemilil Sugar), Ezekiel Otuoma (Ulinzi Stars), Raymond Murugi (KCB FC), John Macharia (KCB FC), Ismael Dunga (Tusker FC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 31 WAITWA KAMBI YA U23 KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top