// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MTIBWA SUGAR YATINGA FAINALI KOMBE LA MPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MTIBWA SUGAR YATINGA FAINALI KOMBE LA MPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, January 10, 2015

    MTIBWA SUGAR YATINGA FAINALI KOMBE LA MPINDUZI

    Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
    MTIBWA Sugari ya Morogoro imetinga fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa penalti 4-3, kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja w Amaan, Zanzibar.
    Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar itasubiri mshindi wa Nusu Fainali ya pili usiku kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Polisi ya hapa ikutane naye katika fainali.
    Kwa mara nyingine leo, kipa Said Mohammed alicheza penalti moja ya Ismail Khamis, wakati ya Mohammed Abdallah ilikwenda nje.
    Waliofunga penalti za Mtibwa Sugar ni Ally Shomary, Henry Joseph, Ramadhani Kichuya na Vincnet Barnabas, wakati za JKU zilifungwa na Isihaka Othman, Issa Khaidary na Khamis Abdallah.
    Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakiwa wamembeba mpigaji wa penalti yao ya mwisho, Vincent Baranabas
    Mchezaji wa JKU, Hilal Refani akiondosha mpira kwenye hatari baada ya Mtibwa Sugar kupiga kona 

    Polisi iliwatoa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 waliokuwa mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda, wakati Mtibwa waliwatoa Azam FC ya Dar es Salaam kwa penalti 7-6 baada ya sare ya 1-1 katika Robo Fainali, huku Said Mohammed akicheza penalti mbili. 
    Katika dakika zote 90 za mchezo wa leo, timu zote zilishambuliana kwa zamu na Mtibwa Sugar walipoteza nafasi tatu za wazi za kufunga kupitia kwa Ame Ally, Mussa Mgosi na Ally Shomary, wakati Amour Omar aliyefunga bao pekee JKU ikiitoa Yanga juzi, leo ‘alifichwa’.
    Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Said Mkopi/Ally Lundenga dk47, David Luhende, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Henry Joseph, Mussa Nampaka/Ibrahim Rajab Jeba dk71, Muzamil Yassin, Ame Ally, Ally Shomary na Mussa Hassan Mgosi/Vincent Barnabas dk62.
    JKU; Mohammed Abdulrahman, Pancian Malik/Mohammed Malik dk33, Suleiman Omar, Issa Khaidary, Khamis Abdallah, Ismail Khamis, David Christopher/Mbaraka Chande dk64/Salum Said dk64, Isihaka Othman, Amour Omar Janja, Hamisi Shaweji na Mohammed Abdallah.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YATINGA FAINALI KOMBE LA MPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top