• HABARI MPYA

  Saturday, January 10, 2015

  PIGO BAFANA BAFANA AFCON 2015, PHUNGWAYO AENGULIWA KIKOSINI BAADA YA KUUMIA GOTI

  Na Mwandishi Wetu, JOHANNESBURG
  BEKI wa Orlando Pirates, Patrick Phungwayo ameenguliwa kwenye kikosi cha Bafana Bafana kitakachoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea baadaye mwezi huu kutokana na majeruhi.
  Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA) limesema leo kwamba mchezaji atakayechukua nafasi yake atatajwa haraka iwezekanavyo.
  Phungwayo aliumia goti wakati wa mazoezi ya mwisho ya Bafana Bafana katika kambi yao fupi mjini Johannesburg Desemba 30 mwaka jana na akakosa mechi ya kirafiki dhidi ya Zambia, ambayo Afrika Kusini ilishinda 1-0 Uwanja wa Orlando, akienda kutibiwa.
  Patrick Phungwayo ameenguliwa kikosi cha AFCON kwa sababu ya maumivu ya goti

  Beki huyo pia alikosa awamu mbili za mazoezi ambazo Bafana ilifanya mjini Libreville, Gabon na leo alipelekwa hospitali kwa ajili ya kipimo cha 
  MRI baada ya madktari wa timu kuona anachelewa kupona.
  Vipimo vimeonyesha kwamba, mlinzi huyo anahitaji wiki kadhaa za kuwa nje kwa mapumziko, ndiyo maana ameondolewa kikosi cha AFCON.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO BAFANA BAFANA AFCON 2015, PHUNGWAYO AENGULIWA KIKOSINI BAADA YA KUUMIA GOTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top